Tuesday, March 29, 2016

ANZA KUPENDA PILIPILI SASA


 Daktari David Heber, Profesa wa Chakula na Lishe nchini Uingereza anasema asilimia 80 ya pilipili kali zote zina kemikali iitwayo "Capsaicin" ambayo ina asili ya kuondoa sumu mwilini. Kemikali hii ndiyo huifanya pilipili kuwa kali.

Pilipili ina uwezo wa kupambana na saratani, utafiti uliofanywa na jopo la madaktari na kuchapishwa kwenye jarida la utafiti wa Saratani unaeleza kuwa kemikali ya Capsaicin inazifanya seli zisababishazo saratani kufa zenyewe.

Kwa mwenye uwezo wa kuila au kupunguza makali yake kwa kiasi fulani anaweza kuitumia kama dawa ya "kipanda uso" na kuondoa mkusanyiko wa makohozi kooni au puani.

Kemikali ya Capsaicin inasaidia kuchoma kalori mwilini hivyo kusaidia kupunguza mafuta ya ziada mwilini, Dawa nyingi za kupunguza unene huchanganywa na kemikali hii inayopatikana katika pilipili.
Pilipili pia imetibitika kuongeza hamu ya ndendo la ndoa kwa kuzalisha vichocheo zaidi.

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home