KUNA HAJA YA KULIANGALIA KWA NAMNA NYINGINE HILI
Wakati rais wetu ndugu Dr john pombe magufuri akijitahidi kkukusanya pesa kwenye idara ya uchumi, ni jambo jema sana kwa hili jambo na ni furaha iliyoje kuona kuwa uhimizwaji wake wa kila mtukudai risiti pale unaponunua bidhaa,lakini jambo ambalo linanipa wasiwasi ni pale maduka mengi huku mikoani hasa maeneo ya wilayani matumizi ya hizi mashine za EFD hakuna kabisa, unakuta mtu ana duka lacement lenye ukubwa wa hadi mil 10-20 lakini ukinunua hata mifuko miwili unaandikiwa risiti ya karatasi, suala je nani ataamini hizi risiti kuwa ndo halali?
Serikali ya awamu ya nne iliimiza sana matumizi ya mashine hizi za TRA kuwa ndio mworobaini kwa wakwepaji wa kodi, je serikali inalitambua hili,katika wilaya yangu ninayotoka nimewahi kuiona duka moja tu, linatumia mashine hizi, ninaweza kusema matumizi ya mashine hizi ni 12% tu basi muhamie wilayani kukagua kuliko kuangalia makao makuu za wilaya.



0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home