Saturday, April 15, 2023

MTIHANI WA SAYANSI DRS VII

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

 

  

 

MTIHANI WA PAMOJA WA UTAMILIFU DARASA LA SABA 

 

JULAI  2019 

 

SAYANSI 

Muda: Saa 1:30  

MAELEKEZO KWA WATAHINIWA 

 

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye maswali arobaini na tano (45) 

 

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.  

 

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika karatasi maalum ya kujibia (OMR) 

 

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR na kwenye ukurasa wenye swali 41 - 45    katika karatasi ya maswali  

 

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika   

  katika fomu ya OMR  

 

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa kila swali katika karatasi yako ya kujibia    OMR kwa swali la 1 - 40. Kwa mfano kama jibu ni D weka kivuli kama ifuatavyo:- 

 

 

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli sio sahihi futa kivuli hicho kwa umakini  kwa  kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya. 

 

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali namba 1 - 40 na tumia kalamu ya wino    wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 - 45 

 

9. Simu za mkononi “HAZIRUHUSIWI” katika chumba cha mtihani. 

 

Karatasi hii ina kurasa 5 zenye maandishi 

   

SEHEMU A Chagua herufi ya jibu sahihi 

1. Ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa wa ngono? [

(a) Kaswende (b) Trakoma (c) Kisonono (d) V.V.U / UKIMWI (e) Trikomona 

2. Ogani inayozalisha kimeny’enya cha fati na mafuta huitwa ………………………..  [ ] (a) moyo (b) figo (c) kongosho (d) ubongo (e) tumbo 

3. Mshipa unaosafirisha damu chafu kwenda kwenye mapafu huitwa …………………… [

(a) ateri (b) vena kava (c) vena (d) ateri ya polimonari (e) vena ya polimonari 

4. Upi ni mpangilio wa sahihi wa uandishi wa ripoti ya Jaribio. [

(a) Njia, Vifaa, Kusudi, Matokeao na Hitimisho  (b) Njia, Vifaa, Kusudi, Hitimisho na Matokeo 

(c) Kusudi, Njia, Vifaa, Matokeo na Hitimisho (d) Kusudi, Vifaa, Njia, Matokeo na Hitimisho  

5. Hatua ya kwanza ya kumhudumia majeruhi wa ajari ni [

(a) Kutibia kwenye jeraha (b) Mpeleke majeruhi hospitali (c) Mtoe majeruhi katika eneo la hatari (d) Kumpatia mchanganyiko wa sukari na chumvi (e) Kuita gari la wagonjwa 

6. Sehemu ipi ya ua inayokuwa na kuwa mbegu baada ya uchavushaji?.  [ ] (a) Ovyuli (b) Ovari (c) Stigma (d) Petali (e) Sepali 

7. Gesi gani inayounda bayogesi kwa kiwango kikubwa? [

(a) Kabonidayoksaidi (b) Uvuke (c) Naitrojeni (d) Oksijeni (e) Mitheni 

8. Homoni inayodhibiti mmeng’enyo wa chakula huitwa……………….  [

(a) Insulini  (b) Parathormoni (c) Adrenalini (d) Thairoksini (e) Oksizitesini 

9. Joto husafiri kwa njia gani katika maada yenye hali yabisi?. [ ] (a) Transilokasheni (b) Msafara (c) Mnururisho (d) Mpitisho (e) Transifomasheni 

10. Sehemu inayolinda ua kabla halijachanua huitwa ……………………… [

(a) Petali (b) Sepali (c) ovari (d) staili (e) kikonyoa 

11. Kipimio kinachothibitisha kuwa damu ina V.V.U huitwa……………  [

(a) Kipimio cha damu (b) Western blot  

(c) Kipimio cha mkojo (d) Kipimio cha malaria (e) Kipimio cha haraka 

12. Upungufu wa vitamin inayozalishwa katika ngozi kwa msaada wa mwanga wa jua husababisha ugonjwa wa …………………….         [ ] 

(a) Kiseyeye (b) Beriberi (c) Pallagra (d) Matege (e) Ukavu macho 

13. Paneli za jua hubadilisha nishati ya mwanga kuwa aina gani ya nishati?  [ ] (a) Umeme (b) Sauti (c) Elektroni (d) Mwanga (e) Joto 

14. Kitendo cha kusafirisha chakula kutoka kwenye majani kwenda kuhifadhiwa huitwa  [

(a) Respiresheni  (b) Transipiresheni  

(c) Transilokesheni (d) Fotothinthesisi (e) Kuota kwa mbegu 

15. Sehemu ipi katika kielelezo kifuatacho inayohusika katika mfumo wa homoni na mmeng’enyo wa chakula?        [ ] 

(a) A  

(b) B  

(c) C  

(d) D  

(e)

16. Tendo la urutubisho hufanyika katika sehemu gani ya via za uzazi wa mwanamke? [

(a) Ovari (b) Uterasi (c) Selviksi (d) Kuta za Uterasi (e) Mirija ya falopia 

 

17. Haemofilia ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa …………………… [

(a) Vitamini B1 (b) Vitamini B2 (c) Vitamini K (d) Vitamini C (e) Vitamini B12 

18. Kifaa kinachotumika kupima mkondo wa umeme katika sakiti huitwa ……………… [ ] (a) Voltimita (b) Amita (c) Galvanomita (d) Ohmmita  (e) Ampia 

19. Sehemu ya seli inayotawala shughuli zote za seli ni …………………. [

(a) Nyukliasi (b) Kiwambo cha seli  

(c) Ukuta wa seli (d) Saitoplazimu (e) Kloroplasti 

20. Kuna maumbo mangapi ya sumaku?  [

(a) 3 (b) 6 (c) 4 (d) 5 (e) 2 

21. Moja kati ya shughuli zifuatazo haisaidii kutunza mazingira yetu, nayo ni …………… [

(a) Kupanda miti  (b) Kujenga uzio  

(c) Kulima kwa kufuata kontua (d) Matumizi mrudio wa takataka (e) kukata miti 

22. Lava wa kipepeo hujulikana kama……………….. [

(a) Funza (b) Kiluwiluwi  (c) Pupa (d) Kiwavi (e) Mdudu kamili 

23. Sehemu ya mfumo wa upumuaji ambayo mbadilishano wa gesi hutokea huitwa? [ ] (a) Trakea au umio wa hewa (b) Pua    (c) Viriba hewa (d) Bronchioli  (e) Bronkasi 

24. Lenzi inayokusanya miale ya mwanga huitwa … [

(a) Lenzi mbinuko (b) Lenzi mbonyeo  

(c) Kioo bapa  (d) Kioo mbinuko (e) Kioo mbonyeo 

25. Ugonjwa unaosababisha na bakteria aina ya basili huitwa …………………….. [ ] (a) Kifua kikuu (b) Kichomi (c) Pumu (d) Kansa (e) Kuhara 

26. Mkono wa binadamu ni nyenzo daraja la ngapi? [ ] (a) Kwanza (b) Tatu (c) Nne (d) Pili  (e) Tano 

27. Sehemu iliyooneshwa kwa herufi K huitwa …………………….  [

(a) Aksoni 

(b) Saitoplazimu  

(c) Mafuta (d) Dendriti  

(e) Nyukliasi 

28. Juma alitumia kani ya N20 kufanya kazi ya joule 50. Tafuta umbali wa uelekeo wa kani? 

(a) m 2.5 (b) m 0.25 (c) m 25 (d) m 1000 (e) m 100 [

29. Ipi kati ya yafuatayo si sababu ya kutoa huduma ya kwanza ……………………….. [

(a) Kuokoa maisha (b) Kupata fedha  

(c) Kupunguza maumivu (d) Kuzuia kutoka kwa damu (e) Kutoa matumaini 

30. Njia ipi inayotumika kuwasilisha data za uchunguzi au utafiti wa kisayansi? [

(a) Uchunguzi (b) Wastani (c) Takwimu kwa duara (d) Umbali (e) Asilimia 31. Sehemu ipi katika kielelezo kifuatacho husukuma damu kuelekea sehemu zote za mwili.  

(a) A  

(b) B   [

(c) C  

(d) D  

(e)

 

 

32. Alama hii inawakilisha nini katika sakiti ya umeme. [

 

(a) Kihisi umeme (b) Fyuzi (c) Mkondo geu (d) Mkondo mnyoofu (e) Kikinza 

33. Ipi ni njia ya asili ya uzazi wa mpango kati ya zifuatazo.  [

(a) Kutumia kondomu  (b) Sindano  

(c) Kuendelea kumnyonyesha mtoto (d) Kutumia vidonge  

34. Sehemu ipi ya mwili inayotengeneza seli zinazoshambuliwa na V.V.U [ ] (a) Uroto mwekundu (b) Moyo (c) Ini  (d) Uroto wa njano (e) Mapafu 

35. Ogani katika kielelezo kifuatacho hutoa taka mwili gani?    [

 

(a) Urea  (b) Jasho  

(c) Mkojo  

(d) Kabonidaioksaidi   

(e) Amonia 

 

36. Muunganiko wa Elementi zisizofanana mbili au Zaidi ya mbili huitwa ……………………. [ ] (a) Molekyuli (b) Valensi (c) Kampaundi (d) Elektroni (e) 

37. Tafuta ukubwa wa pembe akisi (r)  [

 

(a) 350  

(b) 550  

(c) 450  

(d) 300  

(e) 700 

38. Ipi kati ya kazi zifuatazo si kazi ya mifupa.  [

(a) Kutengeneza damu (b) Kuupa mwili umbo (c) Kusimamisha mwili na kutembea  

(d) Kulinda ogani za ndani ya mwili (e) Kupitisha taarifa 

39. Badili 143.60F kuwa sentigredi? [

(a) 600C (b) 630C (c) 59.40C (d) 760C (e) 620C 

40. Sehemu ipi katika kielelezo kifuatacho huonesha Humerasi?  [

(a) C  

(b) B  

(c) D  

(d) A  

(e)

 

   

 

Mkoa_________________________ Wilaya_________________________________ 

 

Shule________________________________________________________________ 

 

Namba ya Mtahiniwa___________________________________________________ 

 

Somo________________________________________________________________ 

SEHEMU B:  

Jibu maswali yafuatayo 

41. Andika mlinganyo ua alama ya kikemikali inayowakilisha maada ambayo inauwezo wa kupatikana katika hali kuu tatu za maada …………………… 

 

42. Tafuta mkondo wa umeme katika sakiti ifuatayo?  

  

43. Mashine ya jitihada ya N250 ilijongea umbali wa meta 16 kuinua mzigo wa N500 kwa umbali meta 

4. Tafuta ufanisi wa mashine. 

 

 

 

 

44. Sehemu ya jicho ambayo inafanana na filamu katika kamera huitwa ……………………. 

 

45. Tafuta thamani ya mzigo X katika mchoro ufuatao:  

  


2 Comments:

At March 8, 2026 at 4:46 AM , Blogger Vanessa said...

Jina langu ni Vanessa Delarue.

Ninatoa ushuhuda huu kuthibitisha uwezo wa mzee wa ajabu.

Nakuhakikishia kwamba niliwasiliana na marabouts kadhaa ambao walikuwa wadanganyifu, waongo, walaghai—sijui niwaite nini tena. Lakini baada ya kutafuta sana, nilikutana na mzee huyu ambaye alinirudishia furaha yangu kweli, furaha ambayo nimekuwa nikitafuta kwa miaka mingi. Yeye ni mzuri sana. Nilikuwa nikiteseka kutokana na kutengana na mume wangu; aliniacha mwaka mmoja na mwezi mmoja uliopita. Hata nilipoteza kazi yangu. Baba yangu alikuwa mgonjwa sana, lakini ndani ya siku tatu, nakuhakikishia, miujiza imetokea maishani mwangu kutokana na mzee huyu. Leo, ninaishi vizuri na mume wangu, baba yangu amepona, niliitwa kurudi kazini, na hata nilikataa, lakini sasa niko katika idara tofauti ambayo ni bora kuliko nyingine. Sijui jinsi ya kumshukuru mzee huyu. Alinifanyia kazi bila kunitoza euro moja. Nilihisi kuridhika kwanza kabla ya kumzawadia. Yeye ni mzuri sana.
Kwa hivyo, ikiwa una tatizo lolote, ikiwa una wasiwasi wowote, usijali tena. Wasiliana na mzee huyu moja kwa moja. Hapa kuna
Anwani yake ya WhatsApp: +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com

 
At March 8, 2026 at 4:47 AM , Anonymous Anonymous said...

Nataka kutoa ushuhuda kuhusu jinsi nilivyopona kutokana na Virusi vya Herpes. Miezi michache iliyopita nilikuwa na dalili kadhaa. Nilienda kumuona daktari na vipimo vingi vya damu vilifanywa kwangu, baadaye niliambiwa nilikuwa na Herpes. Daktari wangu aliniambia kwamba hakuna tiba ya Herpes. Nilijisikia vibaya, niliingia mtandaoni nikitafuta tiba inayowezekana ya Virusi vya Herpes, niliona chapisho la Dkt. Dawn, daktari wa mitishamba anayewasaidia watu kupona kutokana na Herpes. Saratani. VVU na mengineyo. Niliwasiliana naye na kumwambia jinsi ninavyohisi. Alisema dawa yake ya mitishamba inaweza kuniponya. Alinitumia dawa kupitia huduma ya utoaji wa UPS na nilipokea dawa siku 6 baada ya kuituma, nilichukua dawa kama alivyoniagiza. Kabla sijakamilisha dawa dalili zilisimama. Nilienda kwa daktari na kufanya kipimo kingine cha damu, cha kushangaza nilikuwa hasi. Sijapata dalili tena. Dkt. Dawn ni mzuri na unaweza
kuwasiliana kwenye WhatsApp: +2349046229159
Gmail ( dawnacuna314@gmail.com )

Ikiwa unahitaji dawa za mitishamba kutibu magonjwa yoyote sugu au ya zinaa kama.
HERPES.
SARATANI.
VVU/UKIMWI na zaidi

 

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home